Loading...
 

Mikutano yenye Dhamira

 

 

Mikutano yenye malengo ni mikutano maalum ambapo klabu zinazingatia utathmini na jinsi ya kuboresha na kuendeleza vipengele maalum vya hotuba. Mifano michache ni:

  • Lugha ya mwili 
  • Kutembea
  • Utofauti wa sauti
  • Muundo wa hotuba
  • Utumiaji wa visaidizi
  • Utumiaji wa takwimu
  • Utumiaji wa sitiari
  • Utambulisho wa hotuba
  • Hitimisho la hotuba

 

Chaguo nyingi ziwezekanavyo zinawezekana; cha muhimu ni kuzingatia lengo moja kwa wakati. Usijaribu kuwa na mikutano ya kutafuta masuluhisho yote kwa pamoja, mikutano ya namna hiyo inakuwa haina ufanisi.

Mikutano ya malengo ni jukumu la Makamu wa Rais wa klabu.

Utaratibu

1. Maudhui au lengo la mkutano linatangazwa kabla na mtathmini maalum anateuliwa kwa ajili ya mkutano.

2. Mkutano unatumia ajenda ya kawaida, na wanachama wote wanafanya majukumu yao na hotuba zao kama kawaida. Mikutano ya malengo haimaanishi kuwa malengo mengine (haswa yale kutoka mpango wa kielimu) yanatekelezwa au yanabadilishwa. Kwa mfano, kama mwanachama anatakiwa kuwasilisha hotuba ambayo lengo kuu ni utofauti wa sauti, na lengo la mkutano ni kuboresha lugha ya mwili, basi mwanachama anatakiwa kuzingatia vitu vyote.

3. Mwishoni mwa mkutano, mtathmini maalum anawasilisha ripoti. Ripoti lazima imguse kila mmoja aliyekuwa na jukumu lolote lile. Hii inajumuisha kiongozi wa mkutano, wazungumzaji, hotuba za papohapo "waliojitolea",  nk. Ni vigumu kutoa ripoti kamilifu kwa kila mmoja, lakini mtathmini ajitahidi kutoa japo pointi moja au mbili za kuboresha kwa kila jukumu. Kama wanachama wowote walifanya kitu kizuri sana kwenye eneo ambalo walikuwa wanatathminiwa, hilo linatakiwa litajwe, kama mfano kwa wengine. Muda uliopangwa kwa kipengele hiki kinategemea idadi ya washiriki kwenye mkutano. Kwa kawaida, kati ya dakika 5 na 10 zinatosha.

 

 


Contributors to this page: zahra.ak and agora .
Page last modified on Thursday August 12, 2021 10:30:11 CEST by zahra.ak.